Game Mkwanja - Masharti na Vigezo
Utaratibu wa Ushiriki na Masharti ya Kampeni
Jina la Kampeni: Game Mkwanja
Muda wa Kampeni: Miezi 4
Vigezo vya Kushiriki:
- Washiriki lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi.
- Washiriki lazima wawe wateja wa Benki ya CRDB.
- Wafanyakazi wa Benki ya CRDB hawaruhusiwi kushiriki kwenye kampeni hii.
- Washiriki lazima wawe wateja wa rejareja wenye akaunti iliyozuiliwa (dormant) au wawe wamesajiliwa na wanatumia moja au zaidi ya njia za kibenki za CRDB kama vile SimBanking, CRDB Wakala au TemboCard.
- Kwa kushiriki, mteja anakubali kwamba Benki ya CRDB inaweza kuchapisha au kuonyesha taarifa zake binafsi, picha, video, na/au sauti kupitia televisheni, redio, intaneti, na njia nyingine za mawasiliano.
Ushiriki wa Mchezo:
- Kampeni hii inawaruhusu wateja binafsi wa Benki ya CRDB wenye akaunti zilizozuiliwa pamoja na wateja wanaotumia njia za kibenki za CRDB kama SimBanking, CRDB Wakala na Tembocard.
- Wateja wanaostahili kushiriki watapokea SMS yenye kiungo(link) inayowaelekeza kwenye tovuti ya Benki ya CRDB (crdbbank.co.tz) ambapo wanaweza kucheza mchezo na kujishindia zawadi za pesa taslimu.
- Kila mshiriki atacheza mara moja tu kwa kutumia kifaa kimoja (simu janja au laptop) na lazima atumie namba ya simu iliyosajiliwa na akaunti yake ya Benki ya CRDB.
Kwa kushiriki, wateja wanakubaliana na yafuatayo:
- Kucheza kwa uaminifu bila kutumia roboti, programu za otomatiki au mbinu zisizoruhusiwa.
- Kutotumia mapungufu ya mfumo kwa faida binafsi.
- Vitendo vya udanganyifu vinaweza kusababisha adhabu, kusimamishwa au kupoteza zawadi.
Muda wa Kiungo cha Mchezo: Kiungo kwenye SMS kitakuwa hai kwa siku 3. Washiriki wanahimizwa kucheza ndani ya siku hizo 3.
Masharti ya Miamala:
Masharti haya yanawahusu wateja waliotimiza miamala 5 au zaidi yenye jumla ya TSh 50,000/- bila kujumuisha wateja waliolala.
- Washiriki lazima wafanye miamala 5 mfululizo kwa siku 7, yenye jumla ya TSh 50,000/- au zaidi kuanzia Jumatatu hadi Jumapili wakati wa kampeni.
- Wateja lazima wawe wametumia huduma tatu tofauti kutoka njia yoyote kati ya hizi nne: SimBanking, Tembocard, na CRDB Wakala.
Aina za miamala inayokubalika kwa kila njia:
- SimBanking: Miamala yote isipokuwa TV, UTT, Precision Air, SADAKA, manunuzi ya muda wa maongezi, na kuangalia salio kupitia USSD.
- CRDB Wakala: Miamala yote isipokuwa kuweka fedha, GEPG, kununua muda wa maongezi, na malipo ya bili.
- Tembocard: Miamala yote ya ATM, POS na mtandaoni.
Washindi na Zawadi:
- Washindi watathibitishwa kulingana na masharti ya kampeni.
- Washindi watatangazwa kupitia mitandao ya kijamii ya Benki ya CRDB (Facebook, Twitter, Instagram au YouTube), redio washirika, na vyombo vingine vya habari.
- Washindi wanaweza kuombwa kutoa ushuhuda wa kampeni.
- Zawadi zitajumuisha TSh 50,000/-, 100,000/-, na 200,000/- kwa washindi wa kwanza 50 kila wiki, kulingana na idadi ya alama zilizokusanywa:
Uchaguzi wa Washindi wa Wiki:
- Washindi 30 wa kwanza waliokusanya pointi 5,000–9,800 watapokea TSh 50,000/- kila mmoja.
- Washindi 15 wa kwanza waliokusanya pointi 10,000–19,800 watapokea TSh 100,000/- kila mmoja.
- Washindi 5 wa kwanza waliokusanya pointi 20,000 au zaidi watapokea TSh 200,000/- kila mmoja.
- Zawadi zitaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mshindi na atapokea SMS ya kuthibitisha.
- Zawadi zitatolewa kila baada ya siku 5 za kazi tangu kupokelewa kwa SMS ya kiungo cha mchezo.
Kipengele cha Ulinzi wa Taarifa Binafsi:
- Tunakusanya taarifa zako binafsi unapowasilisha maombi na kutumia huduma zetu. Taarifa hizi ni pamoja na jina, mawasiliano, utambulisho, taarifa za kifedha na historia ya miamala.
- Taarifa hizi hutumika kuthibitisha utambulisho wako, kutimiza masharti ya kisheria na kudumisha mawasiliano na wewe kuhusu akaunti zako.
- Tunalinda taarifa zako kwa usalama wa hali ya juu na tunazitunza kwa muda unaohitajika tu.
Kwa kukubali masharti haya:
- Unakubali kukusanywa, kutumika na kushirikiwa kwa taarifa zako na wahusika wa tatu pale inapohitajika kwa utoaji, uboreshaji na uendeshaji wa huduma zetu.
- Hii ni pamoja na kushirikiana na watoa huduma, washirika, mamlaka za udhibiti na taasisi nyingine za kifedha.
- Washirika wetu wote wanalazimika kuheshimu makubaliano ya usiri na ulinzi wa taarifa zako.
Una haki ya:
Kuomba kuona, kusahihisha, kufuta au kuzuia taarifa zako binafsi, pamoja na kupinga matumizi yake.
You might also be interested in
Information and updates
Continue ReadingPrivacy Notice
CRDB Bank Plc operates the website; www.crdbbank.co.tz, which provides financial information services This page is used to inform website visitors regarding our policies with the collection, use, and disclosure of Personal Information if anyone decided to use our website and social media pages.
Continue ReadingProduct Terms and Conditions
These terms and conditions outline the rules and regulations for the use of the bank’s website located at www.crdbbank.co.tz
Continue ReadingRates and Charges
Helping you understand your bank rates and charges for different services
Continue ReadingTerms and Conditions for Simbanking App
Terms and Conditions outline the rules and regulations for using Simbanking App
Continue ReadingWebsite Terms and Conditions
These terms and conditions outline the rules and regulations for the use of the bank’s website located at www.crdbbank.co.tz
Continue Reading