TACATDP

Maelezo

Hii ni programu mahsusi ya benki ya CRDB yenye kutoa  mikopo ya riba nafuu, mafunzo, bima na udhamini kwa  wakulima wa Tanzania, inayofadhiliwa na mfuko wa Umoja  wa Mataifa wa kusaidia nchi kutatua changamoto au athari  za mabadiliko ya tabia nchi (Green Climate Fund) kwenye  sekta ya kilimo kwa mazao ya chakula.

• Kununua au kujenga ghala la kuhifadhi chakula  lililojengwa kwa tofali za udongo zilizokaushwa kwa jua,  chuma au bati. 

• Teknolojia na mbinu za kuepusha upotevu wa mazao na  chakula. 

• Kununua au kujenga nyumba kitalu (Green House). 

• Kujenga bwawa au kuchimba kisima cha maji au kuvuna  maji ya mvua kwa ajili ya kumwagilia shambani. 

• Kununua na kufunga pampu ya umwagiliaji ya kutumia  nishati ya umeme jua (solar). 

• Kilimo cha umwagiliaji wa matone au mitaro  iliyoboreshwa  

• Kulima mazao mchanganyiko au kilimo mseto. 

• Kulima mazao mzunguko. 

• Kilimo cha matuta kupunguza kasi ya maji kwenye  miiinuko au miteremko. 

• Kununua au kuzalisha mbolea ya asili (samadi, mabaki  ya mimea, mabaki ya mazao, taka za vyakula n.k). 

• Kununua mbegu bora inayostahimili ukame  iliyopendekezwa na wataalam. 

• Kulima kilimo kisichotumia udongo (hydroponics) 

• Kulima mazao au miti kinga upepo shambani 

• Teknolojia na mbinu za kuongeza unyevu kwenye  udongo

Mikopo hii ya CRDB inatolewa ili kuongeza uhimilivu wa  athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima wa mazao  ya chakula ili kuwawezesha kumudu teknolojia au kununua  zana/nyenzo bora za kilimo hasa za asili na zenye kulinda  mazingira na kutunza rutuba ya udongo. 

Mkulima yeyote (mmoja mmoja, kikundi, AMCOS, SACCOS),  wa kati, mkubwa) kama anahitaji kununua au kutumia mbinu  bora zenye kuongeza ufanisi na mavuno shambani kwake  anaweza kuomba mkopo huu. Vigezo na masharti ya mikopo  ya benki ya CRDB vitazingatiwa.  

Mikopo wa mtaji wa muda mfupi ambao utalipwa   baada ya mavuno 

• Mikopo ya muda wa kati  

• Mikipo ya muda mrefu

Tembelea tawi la Benki ya CRDB au Wakala 

Tupigie Bure: 0800 008 000 au +255 755 197 700  

au tuandikie barua pepe: [email protected]

Unaweza kupendezwa na