Mkopo wa Green Bond

Maelezo

Green Bond (Kijani Bond Loan) inalenga kutoa mikopo kwenye miradi au  biashara zinazozingatia na kuleta matokeo Chanya kwenye mazingira au  katika kukabiliana na athari za uharibifu za mazingira.

Miradi ya Kijani inajumuisha biashara na shughuli zinazochangia uhifadhi wa  mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali. Miradi inayostahili kupatiwa  fedha za Kijani Bond ni pamoja na:  

• Nishati Jadidifu: Uzalishaji, usambazaji na Manunuzi ya Vifaa  vya mifumo wa Nishati ya Jua, Nishati ya Upepo, Nishati ya Maji,  Nishati ya jotoardhi. 

Kilimo Endelevu: Kilimo chenye cheti cha uthibitisho wa kilimo  endelevu. Mfano: Cheti cha Africert, Ecocert, n.k). Kilimo hifadhi,  Ufugaji samaki kwenye mabwawa/vizimba. 

• Usafiri Safi: Uwekezaji katika vyombo vya usafiri vizivyozalisha  hewa ukaa kama Magari, Bajaji na Pikipiki za Umeme, pamoja na  miundombinu yake. 

• Urejeshwaji taka: Uwekezaji katika teknolojia na mifumo ya  kurejesha taka kwa matumizi mapya ili kupunguza uchafuzi wa  mazingira. 

• Majengo Endelevu: Ujenzi au ununuzi wa majengo Kijani yenye  cheti cha uthibitisho (majengo yanayozingatia matumizi bora ya  Maji, Nishati na vifaa vilivyotumika kulijenga), rafiki kwa mazingira yanayotumia ketnolojia ya kuokoa Nishati na maji. 

• Nishati sanifu: Teknolojia na vifaa vinavyopunguza matumizi ya  Nishati kama mifumo ya taa bora (LED), vifaa vya  kupooza/kuongeza joto matumizi madogo ya Nishati. 

• Uzalishaji na usambazaji endelevu wa maji safi na salama na  usimamizi wa maji taka.

Mtu binafsi, kampuni, au mmiliki yeyote binafsi na taasisi nyingine yoyote  inayotambulika kisheria iliyo na mradi wa kijani /pendekezo la biashara  inaweza kutuma maombi ya mkopo wa bondi ya kijani kulingana na sera ya  mikopo ya benki.

Mkopo wa Kijani Bond utatumika kwa kutuma maombi rasmi kupitia tawi lolote  la mtandao wa benki ya CRDB nchini kote. Michakato mingine ya kawaida ya  ukopeshaji ikijumuisha mchakato wa tathmini na uidhinishaji wa benki  utatumika. 

Inategemea na madhumuni ya mkopo. 

Tembelea tawi la Benki ya CRDB au Wakala Tupigie  

Bure: 0800 008 000 au +255 755 197 700 au tuandikie  

barua pepe: [email protected]

Unaweza kupendezwa na